Mbunge mmoja wa bunge la Ghana ameorodhesha na kutaja baadhi ya majina ya vijiji katika eneo bunge lake ambayo yanashirikisha majina ya sehemu za siri za wanaume na wanawake.
Mbunge Frimpoing Osei alikuwa akitaja majina ya vijiji hivyo wakati akimuuliza swali waziri wa Kawi kuhusu usambazaji wa umeme katika maeneo kadhaa ya eneo la jimbo lake la Abirem.
Aidha, Mbunge huyo alitaja majina ya Etwe nim Nyansa, Kote Ye Aboa na Shua ye Morbor, ambapo tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza ni sehemu za siri za wanaume na wanawake.
Baada ya mbunge kuanza kuyataja majina hayo kila mbunge ndani ya bunge hilo ilibidi kujiinamia na kuuficha uso wake kwa aibu kubwa huku baadhi ya wananchi wa nchi hiyo wakishangaa na kuhoji kuwa hawaja wahi kuyasikia kabla ya kutajwa.
Hata hivyo, inasemekana kuwa majina hayo hutolewa na maselta wa kwanza wa jamii na yanatokana na maisha ya watu.
-
Simiyu: Tunaweza vipi kusema NASA bado ipo?
-
Rais Museveni kuitawala Uganda milele
-
Umoja wa Mataifa walaani bomoa bomoa ya Kibera Jijini Nairobi