Operesheni ya kuwahamisha watu kutoka makazi ya Kibera, Jijini Nairobi imezusha kelele na lawama kutoka pande mbalimbali.

Watalaamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wameitaka Kenya kusitisha mara moja zoezi hilo kwani linakwenda kinyume na haki za binadamu.

Taarifa kutoka ofisi ya kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binadamu OHCHR kwa vyombo vya habari, imesema kuwa zoezi hilo lililoanza tarehe 23 mwezi huu wa Julai litawaathiri zaidi ya wakazi elfu 30 ambao wataachwa bila makao.

Aidha, Wataalamu wa kutetea haki za binadamu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa OHCHR wamelaani vitendo vya kuwatoa watu majumbani mwao kwenye eneo hilo la mabanda la Kibera lililopo kusini magharibi mwa Jiji la Nairobi.

Vile vile, watalaamu hao wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Kenya isitishe zoezi hilo mpaka pale utaratibu wa kisheria na usalama wa kutosha utakapofanyika.

Hata hivyo, Bomoa bomoa hiyo imefanyika kinyume na makubaliano ya hapo awali kati ya Mamlaka ya Barabara za mijini Kenya, Urban Roads Authority, KURA, Tume ya kitaifa ya Ardhi na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Kenya, KNCHR.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julia 28, 2018
Samia Suluhu azindua kiwanda cha Soda Jijini Mbeya