Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameutaka Uongozi wa mkoa wa Mbeya kuweka mpango wa kuyatumia maji ambayo yamechakatwa kutoka kiwanda cha soda cha Pepsi cha SBC Mbeya.

Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kiwanda Kipya cha Soda za Kopo za Plastiki cha Pepsi, SBC Mbeya. ambapo ameupongeza Uongozi wa SBC Mbeya kwa kuajiri Watanzania zaidi ya asilimia 90%.

“Niliyoyaona yamenipa moyo na nimepata mafunzo pia nitakapokwenda kwenye viwanda vingine nitawaelekeza cha kufanya,” amsema Samia Suluhu

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya SBC Tanzania, Foti Nyirenda amemueleza Makamu wa Rais kuwa Kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki kitazalisha kreti 24,000 na pia Kiwanda cha Kuchakata maji taka ambapo kiwanda hicho kinatumia zaidi ya dola laki sita kwa ajili ya shughuli za kutunza na kuboresha mazingira.

 

Umoja wa Mataifa walaani bomoa bomoa ya Kibera Jijini Nairobi
Leonardo amkataa Antonio Conte AC Milan