Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya AC Milan Leonardo ameahidi kupambana na yoyote anaepingana na uwepo wa meneja wa sasa wa klabu hiyo Gennaro Gattuso, kwa minajili ya kutaka kumpa nafasi aliyekua meneja wa Chelsea Antonio conte.

Conte anapigiwa upatu na baadhi ya wadau wa klabu ya AC Milan ili akabidhiwe jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo, jambo ambalo limeibua mtafaruku baina ya viongozi.

Leonardo ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuwa mkurugenzi wa michezo wa AC Milan juma lililopita, amesema hakuna haja ya kuanza kumfikiria meneja mpya katika kipindi hiki, wakati meneja aliopo madaraka, alishasaini mkataba mpya mwezi Aprili mwaka huu.

Leonardo amesema Gattuso ataendelea na jukumu lake kama kawaida na anaamini ataweza kufanikisha malengo yanayokusudiwa na uongozi wa klabu hiyo, kama alivyokubali kabla na baada ya kusiani mkataba mpya.

“Msimamo wangu ni kutaka mkataba wa Gatuso uheshimiwe, halitokua jambo la busara kuuvunja mkataba ambao umesainiwa miezi michache iliyopta, hali hii itaigharimu klabu kiasi kikubwa cha pesa.

“Tunapaswa kuamini aliyekuwepo madarakani ndio alikua chaguo sahihi kwa viongozi, sasa iweje linaibuka suala la mtu mwingine katika kipindi hiki ambacho ni muhimu kwa kila mmoja wetu kwa maslahi ya AC Milan, inayotazamiwa kushiriki ligi kuu kwa ushindani mkubwa.” Alisema Leonardo akiwaambia waandishi wa habari.

Gattuso alilazimika kupandishwa chezo na kuwa meneja wa AC Milan akitokea kwenye kikosi cha vijana cha klabu hiyo, kwa ajili ya kuziba nafasi ya Vincenzo Montella aliyeondoka mwezi Novemba mwaka jana.

Alifanikiwa kupambana na kuiwezesha AC Milan kumaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ya Italia (Serie A), huku akifika hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League.

Kama isingekua adhabu iliyotolewa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA ya kufungiwa kushiriki mcihuano ya bara hilo msimu ujao, Gatusso angerejea tena kwenye michuano ya Europa League akiwa na kikosi cha AC Milan baada ya kuiwezesha timu yake kufuzu.

Samia Suluhu azindua kiwanda cha Soda Jijini Mbeya
Mrema awatangazia kiama wanao mtolea lugha chafu JPM