Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita katika Jimbo lake ambao wamefaulu na kwenda kusoma katika shule mbalimbali nchini.

Kingu amesema kuwa wanafunzi hao wamepata ufadhili huo kupitia taasisi yake ya Kingu Scholarship Program na kuwa tayari wamekwisha lipia ada zao.

“Nimeona ni vizuri wanafunzi wote waliopo katika jimbo langu ambao wanaenda kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na sita niwalipie ada kwani hilo ni moja ya jukumu langu kama mbunge wao” amesema Kingu.

Amesema kuwa katika suala la kuinua elimu ni jukumu la kila mmoja na si kuiachia serikali pekee ambayo ina maeneo mengi ya kushughulikia.

Aidha, amesema kuwa watoto wengi wanauwezo wa kimasomo lakini baadhi yao wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali hivyo wakiachwa bila ya kusaidiwa taifa litakosa wataalamu siku za usoni.

 

Hata hivyo, ameongeza kuwa ameanzisha taasisi hiyo kwa lengo la kuwasaidia watoto wa wakulima ambao watafaulu kidato cha nne na kupata nafasi shule za serikali hapa nchini kuwa watalipa ada zao hadi hapo watakapo maliza masomo yao kwani elimu ndio silaha pekee ya kumkomboa mkulima na mfugaji.

Video: Mwisho wa vishindo vya Makonda, Waliochota Nida waanza kuzitema
Luiz Lula Da Silva kugombea tena Urais Brazili