Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amepokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka kwa wadau wa afya Tanzania Health Promotion Support (THPS) na kuvikabidhi katika hospitali ya Msoga iliyopo jimboni humo.

Akikabidhi vifaa hivyo, mwakilishi kutoka THPS, Dkt. Sisty Moshi amesema kuwa wamewezesha vifaa hivyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta hiyo.

“Katika mradi huu wa kusaidia kuzuia maambukizi mapya ya VVU, kutoa huduma, tiba na msaada wa kisaikolojia kwa ufadhili wa serikali ya Marekani, sisi tunafanya kazi katika mikoa ya Kigoma, Pwani na visiwa vya Zanzibar,”amesema Moshi
Kwa upande wake mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewashukuru THPS kwa msaada huo ambao aliukabidhi kwa uongozi wa hospitali ya Msoga.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 3, 2018
Mwingine Chadema ang'atuka na kujiunga CCM