Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesema miradi mingi ya kimaendeleo imetekelezwa jimboni humo, ikiwemo ile ya kuondoa changamoto ya barabara, maji, umeme, madarasa kwa shule za Sekondari na vituo vya Afya kikiwemo cha Marangu HQ.

Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei.

Dkt. Kimei ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Marangu mtoni, na kueleza kuwa miradi hiyo imefanyika ndani ya kipindi cha miaka miwili na miezi mitano ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema, “tumepokea fedha nyingi katika miradi mbalimbali ikiwemo ya maji na umeme na ujenzi wa kituo cha Afya Marangu HQ jambo ambalo hapo awali hatukuwahi kupata miradi mingi kiasi hicho, fedha hizi zililetwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.”

Sehemu ya Wananchi waliojitokeza kumsikiliza mbunge wao katika mkutano uliofanyika Marangu mtoni.

Aidha, Mbunge huyo pia ameonesha kushangazwa na watu wanaobeza mafanikio ya Serikali ya Rais awamu ya sita kwa kudai inakopa sana, na kusema jambo hilo linatokana na bajeti inayopangwa kuendesha nchi kuwa kubwa, kuliko uwezo wa makusanyo ya ndani.

SOFTCARE wagawa taulo za kike kwa Wanafunzi Sekondari
Trump adai atamaliza vita vya Ukraine kwa siku moja