Kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 nchini Kenya, kijana wa miaka 23 John Paul Mwirigi aliweka rekodi isiyosahaulika kwa kushinda uchaguzi wa kiti cha Ubunge wa Igembe Kusini
Hakuwa hata na fedha za kuweka matangazo ya picha na mabango ya kampeni zake na wakati huo ndo kwanza alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu.
John alisimama kama mgombea binafsi kwenye uchaguzi huo asiye na Chama chochote cha siasa na aliwashangaza wengi matokeo yalipotoka na kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa
Siku ya kuapishwa Bungeni alienda kwa kutumia usafiri wa umma maarufu kama Matatu nchini Kenya au unaweza kuziita Daladala kama upo Tanzania, hii ni kwasababu hakuwa hata na chombo chochote cha moto anachomiliki wala fedha ya kukodi usafiri binafsi.
John Paul Mwirigi alitetea tena kiti chake cha Ubunge na kuchaguliwa kwa awamu nyingine kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na kuendelea kushirikia rekodi ya kuwa mtunga sheria mwenye umri mdogo zaidi nchini Kenya.