Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi rais Magufuli. amepokelewa na katibu muenezi wa CCM, Humphrey Polepole.
“Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa, Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu, Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi,” amesema Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.
Hata hivyo, Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015 ambapo alifanikiwa kushinda nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.