Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Mbwana Makata amefunguka kuwa hana mpango wowote kwa sasa kuondoka Ruvu Shooting bali ataendelea kupambania malengo ya klabu hiyo ambayo ni kurudi katika mashindano ya ligi kuu.
Ikumbukwe kuwa Ruvu Shooting imeshuka daraja msimu huu wa 2022/23 hivyo msimu ujao itashiriki mashindano ya Championship.
Kocha Makata amefunguka: “Siwezi kusema kuwa kisa timu imeshashuka daraja basi na mimi nitaondoka, hapana muhimu kwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya safari yetu mpya kwenye mashindano ya Championship.
“Nitaendelea kuipambania Ruvu mpaka pale ambapo tutafikia malengo japokua kwenye mpira wa miguu lolote linaweza kutokea lakini kwa sasa nachojua ni kuwa tunajiandaa kwa ajili ya safari yetu mpya ambayo endapo tukiitumia vyema basi itaturudisha kwenye mashindano ya Ligi Kuu Bara.”