Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema kama akijiunga na klabu yoyote ya Ligi Kuu Uingereza, basi atahitaji kulipwa kiasi cha paundi laki 6 kila wiki.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Star, Messi amechagua klabu tatu za Uingereza ambazo angependa kuzichezea ambazo ni Arsenal,  Manchester United au Manchester City.

Taarifa zinadai kwamba Messi anaweza kuhama Barcelona kwasababu ya matatizo mengi anayopata ikiwemo kodi na kesi za mahakamani.

Lakini pia kiongozi wa ngazi ya juu ya Barcelona alisema kwamba Messi atacheza Barcelona hadi mwisho wa soka lake.

Lambert Akabidhiwa Kikosi Cha Rovers
Taifa Stars Kuivaa Algeria Kesho Usiku