Mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais , kutokana na kura zilizopigwa.
Kura hizo zimempa nafasi mwanasiasa huyo mpya ambaye amechaguliwa kwa kuungwa mkono kwa zaidi ya asilimia 70.
Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ameweza kumtoa madarakani rais wa sasa, Petro Poroshenko ambaye amekubali kushindwa katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi huo.
Matokeo hayo yanaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa rais Poroshenko na kukataliwa kuanzishwa kwa Ukraine mpya ambayo alikusudia.
“Sitawaangusha, Sijawa rais bado lakini kama raia wa Ukraine, ninaweza kuwaambia nchi zote za Kisovieti kuwa watuangalie sisi, Kila kitu kinawezekana,”amesema Zelensky