Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Cost na aliyekuwa akiichezea clabu ya Newcastle, Cheick Tiote amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla akiwa kwenye mazoezi na klabu yake Beijing Enterprises ya nchini China.

Tiote amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 30 ambapo taarifa zimeeleza kuwa mchezaji huyo akiwa katika mazoezi na klabu hiyo, alianguka ghafla na kukimbizwa hospitali na kupatiwa huduma ya dharura kutokana na hali aliyokuwa nayo.

Tiote kabla ya kuhamia Beijing Enterprises ya china alikuwa akiichezea Newcastle akitoea katika klabu ya FC Twente.

Walinzi wa Netanyahu wavutana na walinzi wa Rais wa Togo mkutanoni
Mbowe azungumzia sauti inayodaiwa anazungumza kimapenzi na Wema