Katika hali isiyokuwa ya kawaida, walinzi wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walijikuta katika mgogoro na walinzi wa Rais wa Togo, Faure Gnassingbé.

Tukio hilo lilitokea jana wakati Waziri mkuu huyo wa Israel alipohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) nchini Liberia, ambapo viongozi hao wawili walitakiwa kufanya mkutano wao kabla, lakini mvutano kati ya walinzi wao ulipelekea kuahirishwa kwa mkutano huo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, mvutano huo uliibuka baada ya walinzi wa Netanyahu kuanza kuwakagua walinzi wa rais wa Togo kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mkutano. Hata hivyo, walinzi wa Rais wa Togo walipinga zoezi hilo dhidi yao hali iliyozua taharuki ya muda baada ya pande hizo mbili kuanza kusukumana.

Aidha, hali ya maelewano ilirejea baadae lakini mkutano wa wakuu hao ulilazimika kuahirishwa hadi ratiba nyingine itakapotolewa.

Katika hatua nyingine, Netanyahu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa lengo kuu la safari yake hiyo ni kudumisha umoja kati ya Israel na Afrika.

Mdee, Bulaya wafunguka walichoamua baada ya kusimamishwa mwaka mmoja
Mchezaji Cheick Tiote afariki dunia