Mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Michael Olunga amejiunga na klabu ya China Guizhou HengFeng Zhicheng kwa kiasi cha shilingi milioni 467.

Olunga amejiunga na klabu hiyo ya China iliyopandishwa daraja akitokea katika klabu ya Djurgadens IF ya Sweden baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana.

Gazeti la The Standard nchini Kenya limeeleza kuwa Olunga alikuwa amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake na klabu aliokuwa akichezea.

Olunga aliye wahi kuchezea klabu ya Gor Mahia na Tusker amekuwa akisakwa na klabu ya Urusi ya CSKA Moscow na Galatasaray ya Uturuki, ambapo tayari Guizhou Zhicheng Hengfeng imetangaza kuwa tayari kutoa kitita cha shilingi milioni 467 zilizodaiwa na Djugardens.

 

Benki ya dunia kuikopesha Tanzania dola milioni 350
JPM: Jengeni kituo cha kupaki magari madogo kimara