Mchimbaji mdogo wa madini, aliyetambuliwa kwa jina la Beatus Joackim mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa Kijenge Arusha, amefariki dunia baada ya kukosa hewa akiwa chini mgodini.
Ajali hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago ambaye ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu kutochukua tahadhari kwa sababu mgodi huo ulisimama kufanya kazi kutokana na sherehe za mwisho wa mwaka 2019 .
Ajali hiyo ilitokea katika mgodi wa Tanzanite Mirereni wilaya ya Simanjiro kwenye Kitalu B kinachomilikiwa na Wilfredy Mareale wenye PML namba 0002818.