Mahakama ya Malindi nchini Kenya, imeondoa dhamana aliyopewa mchungaji Paul Mackenzi ambapo Hakimu Mkuu, Elizabeth Usui amesema mshukiwa amekuwa akiendeleza vitendo vyake eneo la Shakahola – Kilifi, licha ya kuzuiliwa kufanya hivyo na kesi yake itatajwa tena Mei 2, baada ya uchunguzi kukamilika.

Mchungaji huyo, Paul Mackenzie ambaye ni muhubiri wa kanisa la Good news International alikamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya na kuzuiliwa katika kituo cha Malindi, kutokana na mauaji ya watu wanne.

Watu hao, walifariki April 13, 2023 baada ya kudaiwa kulazimishwa wafunge kula na kunywa kwa muda, ili kufariki na kwenda kumuona Mungu wao.

Mshukiwa huyo ambaye amekua akidaiwa kuendesha mahubiri yenye itikadi kali katike eneo la Shakahola, alifikishwa mahakama siku ya Jumatatu Aprili 17, 2023.

Ciro Immobile anusurika kifo Italia
Senyamule ahimiza amani, amuombea Rais Samia