Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, McMaster amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutokea vita kati ya Korea Kaskazini na Marekani.
Korea Kaskazini wiki iliyopita ilitangaza kuwa hivi sasa inaweza kuipiga nchi yeyote ya bara la Amerika kwa kutumia makombora baada ya kufanya jaribio la kombora jipya la balistika lenye uwezo wa kufika katika mabara mengine.
“Kuna njia mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo ukiachilia mbali mapambano ya kijeshi, kwakuwa Korea Kaskazini inazidi kutusogelea, hivyo Marekani inaangalia maeneo nyeti ya kuweka dhana za kujikinga na makombora,” H.R McMaster.
Hata hivyo, Shirika la habari la Reuters limesema kuwa ulinzi huo wa kujihami utahusisha kuwekwa kwa mitambo ya kuzuia makombora ya balistika yenye urefu kwenda juu kama ile iliyokuwa imewekwa Korea Kusini.