Waziri wa madini, Angela Kairuki leo bungeni, Mei 23, 2018 ametolea ufafanuzi swala la kifuta jasho kwa waliokuwa wafanyakazi wa Serikali na kutumbuliwa katika sakata la uhakiki wa vyeti feki lililoibuliwa na Rais John Pombe Magufuli.

Kairuki amesema hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi hao hazikuibuliwa na Serikali ya CCM bali ni kosa la jinai kisheria kwa mtu kutumia cheti cha mtu mwingine kufuzu elimu yake hivyo kilichofanyika kilitakiwa kufanyika hivyo kwa mujibu wa sheria na hata waliopenye katika mfumo kwa njia hiyo walitenda kosa la jinai ”criminal offense”.

”Swala hili lilikuwa ni jinai hauwezi kunufaika hata kama uliweza kupenetrate ukafikia mfumo ukafika hapo ndio maana mheshimiwa rais aliweza kutoa amnest, swala hili halijazalishwa hivi hivi na serikali ya CCM ilikuwa ni criminal offense na ilitakiwa lazima kufanya hivyo.  Amesema Kairuki.

Hoja hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alipoitaka Serikali kutolea maelezo juu ya kifuta jasho kwa waliokuwa watumishi wa Umma waliotumikia taifa kwa miaka zaidi ya 20 na kufukuzwa mikono mitupu.

”Walimu au watumishi wengi waliaanza na cheti cha mtu wakaenda wakasomea taaluma wakafaulu wakasomea taaluma zao wakaenda kulitumikia taifa hili kwa miaka mingi sana”

”Swali ni je, Hivi ni kweli serikali yta CCM inadhani ni sahihi kwa watu ambao wamelitumikia taifa kwa miaka 20 wengine mpaka miaka 30 wengine mpaka miaka 40 waondoke hivi hivi bila hata kupata kifuta jasho?.

Mnamo mwaka jana Rais John Pombe Magufuli aliagiza kufanyika kwa uhakiki wa vyeti feki kutokanana pesa kubwa ya taifa kupotea mikononi mwa watu wasiostahili, Rais aliamua kufanya hivyo kuokoa mabilioni ya pesa ambayo watumishi walikuwa wakijilimbikizia baada ya kubaini uwepo wa watumishi hewa katika sekta mbalimbali za Serikali.

 

 

Babu Tale akabiliwa na shtaka zito, apandishwa kizimbani
Unai Emery ateuliwa kuwa kocha mpya wa Arsenal