Beki wa kati Medhi Benatia, amejiondoa kwa muda katika kikosi cha timu ya taifa lake la Morocco, kwa lengo la kuhitaji muda wa kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 29, hajaridhishwa na nafasi anayoipata kwa sasa katika kikosi cha Juventus, kutokana na upinzani uliopo dhidi ya wachezaji wengine wanaocheza nafasi ya ulinzi.
Benatia ameshacheza katika kikosi cha kwanza cha Juventus mara 14 kati ya michezo 39 msimu huu, na kwa mara ya mwisho alijumuika na wachezaji wengine wa kikoisi cha kwanza michezo mitatu iliyopita
Beki huyo alijiunga na kibibi kizee cha Turin kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich.
“Ni maamuzi magumu, lakini sina budi kuyachukua ili niweze kutimiza lengo la kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.
“Unatakiwa kucheza mara kwa mara, ili kutimiza haja ya kuwa mchezaji mwenye vigezo vya kuitumikia timu ya taifa, ninaamini maamuzi yangu ni sahihi.” Amsema Benatia.