Meli ya ya Kampuni ya Ocean Enterprises Limited ya Zanzibar ijulikanayo kama LCT Rahimu imewaka moto mapema leo ikiwa katika bandari ya Bagamoyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutaja chanzo chake kuwa ni hitilafu ya umeme wakati mafundi wakijaribu kuchomelea mlango wa meli hiyo kwa kutumia umeme wa jenereta iliyokuwa ndani yake.

Aidha, amesema kuwa vyombo vya zimamoto na uokoaji vimefanikiwa kuzima moto huo na kwamba nahodha kwa sasa anahojiwa na vyombo vya usalama ili kupata maelezo zaidi.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa meli hiyo imetokea visiwani Zanzibar na ilikuwa bandarini hapo ikisubiri shehena ya kokoto kwa ajili ya kuipeleka Zanzibar

 

Video: Serikali yaokoa milioni 600 kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi
Video: Ridhiwani afunguka kuhusu Polepole kushambuliwa