Nyota wa Filamu za Bongo Menina  amesema kuwa  hawezi kusema kiasi cha pesa anancholipwa  kwenye  kazi  anazopewa na makampuni mbalimbali uigizaji au matangazo.

Akizungumza Kwenye Exclusive interview na Dar 24 msanii huyo anaetamba kwenye tamthilia ya Kiswahili inayokwenda kwa jina la Tandi, amedai kuwa hawezi kusema dau lake, kwani hatua hiyo inaweza kusababisha matabaka katika tasnia, hasa kwa wale waigizaji wapya.

“Siwezi nikasema kwasababu ,unaposema unaweka kama matabaka wengine wanatamani kufanya kazi na wewe inamana hiyo its more  private ukutane mtu na mtu yani kama kuna deal imekuja mezani muongee , kila mtu ana level zake za malipo,” Alisema Menina .

Mwanadada huyo ambaye mwanzo alijulikana sana kupitia muziki wa Bongo Flava akiwa kama mmoja wa washiriki wa shindano la Bongo Star Search, amefunguka kuwa anafurahishwa sana na kile anachokifanya kwa sasa katika sanaa ya uigizaji.

Bofya hapa kutazama ..

Tshishimbi anukia AS Vita
Chato - Nyabilezi, Igando yanufaika kwa mawasiliano