Mwanasoka raia wa Argentina Lionel Messi amezungumzia mpango wake wa kuacha kuichezea timu yake ya taifa endapo wakishindwa kuibuka mabingwa katika michuano ya komba la dunia mwaka huu mwezi Juni nchini Urusi.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona ambaye aliisadia timu yake ya taifa kufunzu mashindano hayo kufuatia kuifungia mabao 3-1 dhidi ya Ecuadoe Octoba, 2017 ameweka wazi kuwa endapo yeye na wachezaji wenzake katika kizazi chao wakishindwa kuchukua ubingwa huo atalazimika kujiengua katika kikosi cha timu ya taifa.
“Tunahisi hivyo, kama tusipo shinda kombe la dunia Urusi, njia pekee itakuwa nikuachana na timu ya taifa” .
Hayo yamezungumzwa na Messi wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha runinga cha La Cornisa.
Aidha, Mchezaji huyo amesema ndoto zake ni kushinda kombe la dunia na kuwa kama Brazil ambao wameshinda kombe hilo mara nyingi zaidi.
Messi mwenye umri wa miaka (30), ameifungia mabao 61 timu yake ya taifa katika michezo 123 aliyo cheza katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina.