Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega, amesema kuwa siku za wanaoagiza nyama, maziwa na samaki kutoka nje ya nchi, zinahesabika kutokana na nchi kuwa na mifugo ya kutosha kama vile Ngombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Punda na hivyo Taifa kama Tanzania halina sababu yoyote ya kuagiza nchi za Nje.

Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma ya kutembelea Mwalo wa Samaki wa Muyobozi Uliopo Wilayani Uvinza, Mwalo wa Kibirizi na kituo cha Taasisi ya Tafiti za Uvuvi Tanzania TAFIRI Kigoma.

“Sioni kwanini tuagize nyama na maziwa toka nje ya nchi, hatuwezi kuendelea kuangiza nyama, maziwa na hata mazao ya uvuvi, kwa nini tusiwekeze katika rasilimali zetu za ndani katika mifugo na samaki na kuongeza pato la taifa? “Amehoji Ulega

Amesema kuwa Wizara yake haitawavumilia wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa hizo nje ya nchi kwani sekta ya mifugo na uvuvi ni sekta ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katika taifa.

Aidha, Ulega ameitaka TAFIRI kuhakikisha wanawafikia wafugaji wa samaki kwa kufanya tafiti zao ili kujua changamoto wanazokutana nazo na kujua namna ya kuzitatua, akitolea mfano wa chakula sahihi kinachotakiwa kupewa samaki wanaofugwa na kuangalia miundombinu ya kufugia.

Hata hivyo, Ulega ameongeza kuwa Wizara yake ina mpango wa kuimarisha eneo la tafiti kwa kuongeza rasilimali fedha kwa kukarabati miundombinu na kuongeza rasilimali watu.

Necta yafanya mabadiliko mtihani darasa la saba
Messi adai kuachana na timu ya Argentina