Mshambuliaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa FIFA katika hafla iliyofanyika Jijini Milan, nchini Italia.
Messi amewashinda Cristiano Ronaldo wa Juventus na Virgil van Dijk (NED) wa Liverpool alioingianao fainali katika kinyang’anyiro hiko.
Kwa upande wa wanawake, Megan Rapince wa Reign FC na timu ya taifa ya Marekani ndiye mchezaji bora akiwashinda Lucy Bronze (ENG) wa Olympique Lyonnais na Alex Morgan (USA) wa Orlando Pride
Tuzo nyingine zilizotolewa ni kama ifuatavyo.
Tuzo ya kocha bora kwa timu za wanaume imekwenda kwa Jurgen Klop wa Liverpool akiwashinda Pep Guardiola wa Manchester City na Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur.
Jill Ellis aliyekuwa akiinoa Marekani ameshinda tuzo ya kocha bora wa timu za wanawake akiwabwaga Phil Neville wa Uingereza na Sarina Wiegman wa Uholanzi.
Tuzo ya shabiki bora imekwenda kwa Silvia Grecco wa Brazil akiwashinda Justo Sanchez wa Uruguay pamoja na Mashabiki wa timu ya taifa ya Uholanzi kwenye Kombe la Dunia kwa Wanawake.
Mbrazil Alisson anayecheza Liverpool ametwaa tuzo ya Golikipa Bora akiwapiku Ederson wa Manchester City na Marc-André ter Stegen wa FC Barcelona.
Tuzo ya golikipa bora wa kike imechukuliwa na Sari van Veenendaal wa Uholanzi aliyekuwa Arsenal sasa Atletico Madrid Sari amewashinda Christiane Endler wa PSG na Hedvig Lindahl wa Chelsea / Wolfsburg.
Tuzo ya goli Bora imekwenda kwa Dániel Zsóri kwenye mchezo kati ya Debrecen FC v Ferencváros TC Februari 16, 2019.
Zsori amewashinda Lionel Messi pamoja na Juan Fernando Quintero.
Tuzo ya mchezo wa kiungwana imekwenda kwa Marcelo Bielsa pamoja na kikosi cha Liverpool .