Nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Dunia Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi, amewashukuru watu wote waliomuwezesha kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka 2022 wa FIFA.
Messi alitangazwa kushinda Tuzo hiyo usiku wa kuamkia leo katika Hafla Maalum iliyofanyika jijini Paris Ufaransa, akiwashinda Kylian Mbappe na Karim Benzema.
Mshambuliaji huyo wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa PSG, amesema amefurahi sana kuwa mshindi wa Tuzo hiyo, pia amefurahia kuona Kocha Mkuu wa Argentina Lionel Scaloni akitajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Kocha Bora wa mwaka 2022.
Pia amempongeza Mlinda Lango wa kikosi cha Argentina Emiliano Martinez kwa kushinda Tuzo ya kipa Bora wa mwaka 2022.
“Asante kwa kila mtu aliyeniwezesha kushinda Tuzo hii (Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka 2022 wa FIFA). Pongezi kwa washindi wote hasa kwa kocha Lio Scalon, kipa Emiliano Martinez na wote ambao walistahili Tuzo” amesema Lionel Messi
Washindi wengine wa Tuzo za FIFA mwaka 2022
Mchezaji Bora Mwanamke: Alexia Putellas
Kipa Bora Mwanaume: Emiliano ‘Dibu’ Martinez
Kipa Bora Mwanamke: Mary Earps
Kocha Bora Mwanaume: Lionel Scaloni
Kocha Bora Mwanamke: Sarina Wiegman
Goli Bora (FIFA Puskás Award): Marcin Oleksy
Tuzo Bora ya Mashabiki: Mashabiki wa Argentina
Tuzo ya uungwana (FIFA Fair Play Award): Luka Lochoshvili
Tuzo ya Hehsima: Pelé
Kikosi Bora Wanaume: Thibaut Courtois; Achraf Hakimi, Joao Cancelo, Virgil van Dijk; Kevin De Bruyne, Luka Modric, Casemiro; Lionel Messi, Kylian Mbappe, Karim Benzema na Erling Haaland.
Kikosi Bora Wanawake: Christiane Endler; Lucy Bronze, Maria Leon, Leah Williamson, Wendy Renard; Alexia Putellas, Keira Walsh, Lena Oberdorff; Alex Morgan, Sam Kerr na Beth Mead