Imeelezwa kuwa Staa mpya wa Klabu ya Inter Miami, Lionel Messi atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi ndani ya kikosi cha klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Marekani.

Ripoti zinaeleza kuwa, Messi atakuwa akilipwa dola Milioni 150 kwa miaka miwili na nusu ambapo fedha hiyo itakuwa ikipanda.

Messi amesajiliwa na Klabu ya Inter Miami ambayo inamilikiwa na staa wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, David Beckham.

Staa huyo ametua hapo akitokea katika Klabu ya Paris Saint-Germain ambako alidumu kwa misimu miwili baada ya kuachana na Barcelona.

Messi aliamua kutua huko licha ya kuwekewa mkwanja mrefu na klabu za Saudi Arabia, lakini amechagua kucheza Ligi Kuu ya Marekani.

Msimu ujao, Messi atakuwa ndani ya Inter Miami ambapo atacheza kwa mara ya kwanza nje ya Bara la Ulaya tangu aanze maisha yake ya siku hivi sasa akiwa na miaka 35.

Kuondoka kwa Messi ndani ya Ulaya, inakuwa ni historia nyingine kwani ni mara ya kwanza msimu ujao michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itachezwa bila ya uwepo wake wala Cristiano Ronaldo tangu mwaka 2003.

Meya na wenzie kizimbani kwa uhujumu uchumi Tanga
Vipimo, utafiti: Hakuna mgonjwa hata mmoja - Dkt. Kaniki