Mlinda Lango Metacha Mnata leo Jumanne (Januari 17) amewaaga wachezaji na Maafisa wa Benchi la Ufundi la Singida Big Stars, Kabla ya kuanza safari ya kuelekea Dar es salaam kujiunga na Young Africans.

MEtacha amesajiliwa na Young Africans kwa Mkataba wa Mkopo wakati wa Dirisha Dogo lililofungwa Januari 15, 2023, ili kuziba nafasi ya Mlinda Lango namba mbili wa Abuutwalib Mshery, ambaye ana majeraha ya muda mrefu.

Young Africans imemrejesha Metacha baada ya msimu mmoja na nusu tangu iachane naye kwa utovu wa nidhamu mwaka 2021, na kutimkia Polisi Tanzania akicheza msimu mmoja kisha kujiunga na Singida Big Stars.

Mlinda Lango huyo ameonekana akifurahia na wachezaji wenzake, makocha na baadhi ya viongozi huku pia akipiga stori na kufurahi na kocha wa timu hiyo, Hans Van De Pluijm licha ya tetesi za awali kuelezwa kuwa kocha huyo hakushirikishwa kwenye uhamisho wa mchezaji huyo.

Metacha alikuwa Mlinda Lango chaguo la kwanza Singida Big Stars baada ya kujiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Polisi Tanzania, uhamisho ambao ulizua utata na kusababisha Singida BS kupewa adhabu ya kufungiwa kusajili japokuwa baadae adhabu hiyo iliondolewa.

Jafo ataka sheria za Mazingira ziheshimiwe
Mkutano wa Jukwaa la Dunia la Uchumi waanza mjini Davos