Kikosi cha Simba SC kimewasili salama jijini Dar es salaam kikitokea Dubai-Falme za Kiarabu, kilipokuwa kimeweka Kambi ya majuma mawili.

Simba SC iliweka Kambi Dubai kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ pamoja na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi.

Kikosi cha Klabu hiyo kilichoanza safari majira ya asubuhi mjini Dubai, kimewasili jijini Dar es salaam majira ya Mchana, na moja kwa moja kimekwenda kambini, tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City FC.

Miamba hiyo itacheza kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Simba SC ikiwa na kumbukumbu ya furaha ya ushindi wa 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbeya City wao hawatohitaji kurejea makosa, kufuatia kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Azam FC kwa kufungwa 6-1, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Serikali yaagiza kufutwa kwa Kampuni ya Parachichi
Ajali ya Ndege Nepal: Familia zakabidhiwa miili ya wapendwa wao