Serikali nchini, imeagiza kufutwa kwa Kampuni ya ununuzi wa parachichi ya Kandia Fresh na kufungiwa kibali cha kujihusisha na ununuzi wa zao hilo, kutokana na kuhusika na parachichi zilizotupwa dampo Mkoani Njombe.

Agizo hilo, limetolewa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akiwa katika kituo cha kuhifadhi Parachichi kilichopo Kijiji cha Nundu mkoani Njombe.

Zao la Parachichi likiwa sokoni Mkoani Njombe.

Akiwa Kijijini hapo, Waziri Bashe pia alikutana na msimamizi wa kampuni hiyo, David Baraza na kuagiza mamlaka za usalama kumshikilia kwa mahojiano.

Aidha, Waziri huyo pia amepia marufuku wakulima kuuza parachichi ambazo hazijakomaa, kwa kuwa zinaua soko la parachichi la Tanzania Kimataifa na kuwataka viongozi wa mkoa wa Njombe kusimamia zoezi hilo.

Mkutano wa Jukwaa la Dunia la Uchumi waanza mjini Davos
PICHA: Simba SC yawasili Dar es salaam