Mfumo wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma Kielectoni -NeST, unatarajia kuondoa tatizo la Rushwa kutokana na mchakato wote wa ununuzi kufanyika kimtandao hivyo kuondoa upotevu wa fedha za Serikali na kuchangia ukuaji wa maendeleo kitaifa.

Akizungumza na wadau mbalimbali wakati akifungua mafunzo ya Ununuzi wa Umma, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma – PPRA Eliakim Maswi, ameziomba asasi za kiraia na wadau kushirikiana na kutoa taarifa pindi ununuzi unapofanyika kinyume na taratibu, ili kuchukua hatua kwa maslahi ya Taifa.

Amesema, “tutoe taarifa kwa mamlaka zinazoshuighulikia Rushwa pia nasi tunayonafasi ya kupokea taariofa na tutalifanyia kazi mfumo huu mpya umzezingatia suala hilo si kupunguza tu bali kuondoa tatizo la Rushwa kwenye ununuzi wa Umma kwa sababu mfumo unafanya mchakato wote tangu mwanzo mpaka mwisho.”

Aidha, Maswi ameongeza kuwa, “tupo tayari kushirikiana na mtu yeyote pindi kitu kinaenda ndivyo sivyo kwa manufaa ya Taifa hili mtanzania mwenzetu utusaidie kutoa taarifa kuhusu ununuzi wa Umma unavyofanyika na sisi tutachukua hatua kwa sababu ni wajibu ambao tumepewa ili ununuzi wa Umma uendane na vile inavyohitajika.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi kutoka Global Peace Foundation – GPF, Dkt. Fatma Waziri amesema mfumo huo mpya utawezesha kuisaidia Serikali kudhibiti ubadhirifu wa fedha uliokuwa unafanywa kabla ya mfumo huo na asasi za kiraia kuwa sehemu ya jicho la pili kwa upande wa Serikali.

Awali, Mkurugenzi wa Peace and Hope ya jijini Mwanza, Augustine Nyakatoma alisema mfumo huo ni mzuri na unaonesha uwepo wa mafanikio mbeleni iwapo wahusika watautumia kwa usahihi kitu ambacho kitasaidia pia kuziba mianya ya rushwa, hivyo watu waaminifu wanahitajika ili kuisaidia nchi kupiga hatua.

Benchikha kusajili mshambuliaji Simba SC
Young Africans hawataki maskhara