Ripoti ya uchunguzi ulifanywa na Shirika la Msaada la World Vision, umebainisha kuwa viwango vya juu vya mfumuko wa bei na kuongezeka kwa gharama za maisha kunachangia uwepo wa njaa Duniani.
Ripoti hiyo, iliyofanyika kwenye Mataifa 16 yaliyoidhinishwa umebaini kwamba asilimia 59 ya wazazi waliohojiwa walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na njaa kwa watoto, pamoja na utapiamlo kwa familia zao.
Aidha, ripoti hiyo pia ilibainisha kwamba asilimia 46 ya familia hizo hazijui wapi pa kupata fedha za kununulia chakula hali ambayo imewafanya wengi kukata tamaa na kusubiri kudra za wahisani.
Rais wa World Vision, Andrew Morely amesema hata kiwango cha watoto wanaolala bila ya kula kimepanda hadi asilimia 38 katika Mataifa ya kipato cha chini, ingawa ameonya kwamba njaa ni tatizo la ulimwengu.
Hatua hii inakuja huku Ulimwengu ukitarajia kuadhimisha Siku ya Chakula, Jumatatu ijayo Oktoba 16, 2023.