Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini – TANESCO, Mhandisi Isima Nyamhanga amesema mgao wa umeme unatarajia kuisha mwishoni mwa mwezi wa tatu, kutokana na jitihada za kukamilisha na kurekebisha kwa haraka baadhi ya vyanzo vya umeme vitakavyosaidia kuongeza upatikanaji wake.
Nyamhanga ameyasema hayo wakati akizungumzia mikakati ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa umeme nchini, ambapo kwa sasa matumizi yaje yameongezeka kwa asilimia 12, hivyo kupelekea kuongezeka kwa changamoto mbalimbali za hitaji hilo.
Amesema, “mikakati yetu iliyopo ni kukamilisha matengenezo katika baadhi ya vituo vyetu Vya uzalishaji wa ume.e vyenye changamoto ambavyo vilipelekea upungufu wa uzalishaji Megawatt 400, hii itasaidia kupunguza tatizo lililopo.”
Mapena hivikaribuni, TANESCO ilitakiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu mgao wa Umeme kutokqnq na baadhi ya wananchi kukumbana na changamoto ya mgao wa umeme kwa muda mrefu jambo ambalo linawaathiri kbiashara na shuguli nyingine za kiuchumi.