Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema nchi yake imekuwa ikiwapokea wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa zaidi ya miaka 20, na kwamba hataweza kuendelea kutoa makazi kwa wakimbizi toka nchi ambayo huwanyimwa haki raia wake.

Kagame ameyasema hayo kupitia hotuba take aliyoitoa kupitia video wakati akiwahutubia Maseneta, na kudai kuwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia iache kuishutumu Rwanda kwa matatizo hayo ikiwemo kuliunga mkono kundi la waasi la M23, na kwamba waasi hao warudi mahali walipotoka.

Amesema, “Kuna kundi moja la wakimbizi ambalo nadhani hatutaruhusu kuwapokea. Hatuwezi kuendelea kutoa makazi kwa wakimbizi wanaokuja kwa sababu ya utakasaji wa kijamii katika nchi nyingine na kuwa sehemu ya kutupa watu hao ambao wananyimwa haki zao.”

Kambi ya wakimbizi ya Mahama nchini Rwanda Rwanda. Picha ya VOA.

Kagame ameongeza kuwa, “Wakati tulikuwa bado na uhusiano mzuri na rais wa sasa wa DRC, nilizungumzia swala hili alipoingia tu madarakani. Nilimwambia kwa kirefu kuhusu swala la wakimbizi likiwemo namna ya kumaliza suala la wakimbizi kuwafanya kuwa raia wa Rwanda lakini Wakimbizi hao hawataki uraia tuliokuwa tunapendekeza kwa sababu wanataka kurudi nyumbani kwao DRC.”

Amesema kwamba Rwanda imejaribu kutoa maelezo ya kutosha kila mara kwamba waasi wanaopigana mashariki mwa DRC hawakutoka Rwanda na kudai kuwa “Wanaotoa madai hayo wanasema hawa ni Watutsi kutoka Rwanda, hata kama ilikuwa miaka 100 iliyopita, na kwamba lazima warudi Rwanda.”

Mamlaka yatoa nauli mpya Mwendokasi, Taxi
Ajali ya Lori, Gari dogo yauwa wanne wa familia moja