Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, amekutana na udhalilishaji akita jukwaani baada ya kundi kubwa la wananchi wanaomsikiliza kumzomea akifanya kampeni katika kaunti yake ya nyumbani ya Kitui mnamo Ijumaa, Juni 17, 2022.
Kalonzo alilazimika kuvumulia udhalilishaji katika soko la Ikutha, eneo la bunge la Kitui Kusini alipozomewa mara kadhaa na kulazimika kukatiza hotuba yake.
Umati huo uliotamka ‘kwenda huko’ ulimfokea Kalonzo ukipinga juhudi zake za kumfanyia kampeni mbunge wa Kitui Kusini na mgombea wa chama cha Jubilee Racheal Kaki Nyamai na kusisitiza kuwa mgombea wa ODM Onesmus Mumo King ndiye awe wa kuzungumza badala yake.
Wakati hayo yakiendelea, Mgombea mwenza wa William Ruto kupitia tiketi ya UDA Rigathi Gachagua nae alipatwa na butwaa alipokuwa akifanyia kampeni ya Muungano wa Kenya Kwanza katika eneo la Githunguri, Kaunti ya Kiambu.
Gachagua alikuwa na wakati mgumu kutuliza umati baada ya kuwashambulia Rais Uhuru Kenyatta na Azimio La Umoja One na mgombea urais wa chama cha Muungano wa Kenya Raila Odinga.
Baadhi ya umati ambao haukutaka kusikia lolote walielezea kukerwa kwao na mashambulizi yake dhidi ya wawili hao na kumshutumu kwa kutomuheshimu rais na Raila.