Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ameshtushwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Yury Fedotov ambaye kwa muongo mmoja alihudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa, inayohusika na madawa na uhalifu UNODC.

Kupitia taarifa iliyotolewa hii leo Juni 18, 2022 na msemaji wake kwa waandishi wa Habari mjini New York Marekani, Guterres amesema wakati wa uhai wake kwa muda wote alipoiongoza ofisi ya UNODC Fedotov alidhihirisha umakini katika kuzisaidia nchi wanachama kumaliza tofauti zao.

“Sambamba na kuzisaidia nchi wanachama kumaliza zilizokuwepo baina yao lakini pia Fedotov alishirikiana katika mchakato wa moja ya kutatua masuala magumu na yeti ya ajenda za kimataifa,” amesema Guterres.

Katibu Mkuu huyo pia ameongeza kuwa, mtazamo na mchango wa marehemu Fedotov kama mshiriki kwenye kundi la utawala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa, ulithaminiwa sana.

Tayari UN imetuma salamu za rambirambi kwa familia ya Fedotov na wapendwa wake wote huku akisema kuwa mchago wake, dhamira yake na kujitolea kwake kwenye Umoja wa Mataifa kuliteta mabadiliko na tija na kwamba mchango utaenziwa na kukumbukwa daima.

Maagizo sita ya Majaliwa ukamilifu anuani za makazi
Mgombea Urais Kenya azomewa nyumbani kwake