Waziri wa nchi Nchi, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemevu, Jenista Mhagama  leo bungeni amewasilisha muswada  wa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma wa mwaka 2018 na kupendekeza kuunganishwa mifuko ya pensheni ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili kuanzisha mfuko mmoja wa hifadhi ya jamii.

Amesema hatua ya kuunganisha mifuko ya pensheni ni kukidhi kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi ili kupunguza gharama za uendeshaji.

Sheria itayopendekezwa itaweka mfumo madhubuti utakaomhakikishia mwananchama kulipwa mafao ya msingi kama inavyoeleza katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara 11 (1).

Ameongezea kuwa sheria hiyo itakuwa na jumla ya mafao 7 yatayolipwa na  mfuko huo yakiwemo, fao la pensheni, faio la warithi, fao la ulemavu, fao la uzazi, fao la ukosefu wa ajira, fao la ugonjwa na fao la kufiwa.

Kiwango cha uchangiaji kitakuwa 20% ambapo mwajiri atachangia 15% na mwajiriwa tachangia 5% ya mshahara wake.

Pia kutakuwa na mfumo amdhubuti utakao hakikisha mwananchama anapata mafao yake kwa wakati, ikiwemo kumlipa mwanacham aliyekidhi vigezo.

Kuanisha adhabu ya tozo ya 5% kwa mfuko utakaochelewesha mafao ya wanachama.

Aidha amefafanua kuwa kupitia Sheria hii itamuwezesha mwanachama kujipatia mikopo ya nyumba na shughuli nyingine za kiuchumi kwa riba nafuu.

Ufafanuzi huo umetolewa leo januari 30, 2018 bungeni.

.

 

Mahojiano Yamponza Khalifa Mgwira
Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi