Mhubiri wa Kanisa la Jesus Revelation Center kutoka kata ya Tezo maeneo ya Mbuyuni nchini Kenya anatarajiwa kufikishwa Mahakamani hii leo kwa tuhuma za kushiriki ngono na mtoto mwenye umri wa miaka 14.

Mchungaji huyo ambaye amezua mijadala mitandaoni kwa kitendo hicho, atafikishwa ili kusomewa shitaka lake huku waumini wake nao wakikumbwa na butwaa kutokana na mfululizo wa matukio ya wahubiri kukubwa na kashfa nzito.

Wakati hilo likitokea, tayari Mchungaji Ezekiel Odero ambaye alihusishwa kushiriki mauaji ya halaiki yaliyotokea shambani mwa Mchungaji mwingine Paul Mackezie wa Kaunti ya Kilifi ameachiwa huru kwa dhamana.

Kwa upande wa Mackenzie yeye alitarajia kupanda kizimbani hii leo kusomewa mashitaka yanayomkabili ya mauaji ya watu zaidi ya 120, akituhumiwa kuwahubiria na kuwataka wafunge kula hadi kufa ili wakakutane na MUNGU wao na huku akiwaaminisha mwisho wa Dunia ni mwaka huu 2023.

Robertinho afunguka makosa ya Ally Salim
Kocha Tanzania Prisons azitaka alama tisa Ligi Kuu