Serikali ya Jmhuri ya Muungano wa Tanzania imetimiza miaka 60 ya ushirikiano na Marekani, ambapo Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Marekani katika nyanja mbalimbali za maendeleo kama ilivyokuwa katika kipindi miaka 60 iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema ushirikiano baina ya mataifa hayo ni wa muda mrefu ambapo viongozi wakuu wa Marekani na Tanzania wamekuwa wakishirikiana kusaidia maendeleo ya watanzania.
Marekani imekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya afya hapa nchini na kupitia shirika lake na USAID linalotekeleza miradi kadhaa ya kiuchumi kwa wananchi.
Aidha, amesema maadhimisho ya miaka 245 ya uhuru wa Marekani na miaka 60 ya ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani ni kielelezo cha ushirikiano usio na mashaka baina ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright amesema Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania kuinua uchumi, kuboresha miundombinu ya barabara, afya na nishati.