Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kwa sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho kusaini Mkataba wa ushiriki katika Eneo huru la Biashara barani Afrika AfCTA.

Ameyasema hayo leo Juni 28, 2021 Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya eneo huru la biashara Afrika (AfCTA) Wamkele Meneambae yupo nchini kwa ziara maalum.

Waziri Mulamula amesema Serikali ya Tanzania inategemea kunufaika na soko la bidhaa zake katika masoko ya nje baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa ushiriki katika Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA).

“Lengo la ziara ya Mhe. Mene hapa nchini pamoja na mambo mengine ni kukutana na viongozi na wadau wengine muhimu kujadiliana na masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba wa AfCTA ikiwa ni pamoja na umuhimu wa Tanzania kuridhia Mkataba huo,” Amesema Balozi Mulamula.

Ameongeza kuwa, uanzishwaji wa AfCTA ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa ambapo pamoja na mambo mengine, utekelezaji wake unatarajiwa kuongeza wigo wa fursa nafuu za biashara nchini kwa kuwavutia wawekezaji na kuongeza mauzo hasa ya bidhaa za kilimo.

Naye Katibu Mtendaji wa Sekretariati ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Mene ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imempatia tangu wakati wa uchaguzi hadi sasa na kuahidi kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utanufaisha kila Nchi Mwanachama.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 29, 2021
Prof. Mkumbo: Azindua maonyesho ya saba saba rasmi