Rais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ina zaidi ya wagonjwa 100 wa Covid-19 ambapo amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya AFya ili idadi hiyo isiongezeke zaidi.

Amesema hayo leo Juni 28, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya mbalimbali yaliyoulizwa na wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wa tathimini ya siku 100 tangu aapishwe kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Amesema kuwa ugonjwa huo upo Tanzania na kuna wagonjwa  wanaendelea kupata matibabu, wengi wanatibiwa kwa kutumia gesi kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

“Nataka niwe mkweli, Tanzania tuna wagonjwa katika hili wimbi la tatu. Mpaka taarifa nilizozipata juzi, nadhani kuna wagonjwa kama 100 na…, kati yao si chini ya 70 wako kwenye matibabu ya gesi, wengine wako kwenye matibabu ya kawaida,” amesema Rais Samia.

“Watanzania wengine wameshakwenda kuchanja wapo waliokwenda Dubai, Afrika Kusini…kwa hiyo tukasema chanjo zije ili watu wachanje kwa hiari,” amesema Rais Samia.

Prof. Mkumbo: Azindua maonyesho ya saba saba rasmi
TBS yasisitiza matumizi huduma zenye ithibati