Mahakama ya Wilaya ya Njombe imemuhukumu Bright Peter Dismas (25) Mkazi wa Kitisi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya makosa mawili likiwemo la ubakaji na kumpa ujauzito mwanafunzi.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Isack Mlowe, ambapo amesema Mshtakiwa huyo alimbaka Mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17 wa Shule ya Sekondari Mkilima iliyopo mjini Makambako.
Amesema tukio hilo la ubakaji lilitokea mwaka jana mwezi February “Mshtakiwa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na Mwanafunzi huyo ambapo siku ya tukio alikwenda nyumbani kwao akiwa peke yake, aliingia ndani na kuandaliwa chakula na Mwanafunzi huyo kisha baadaye wote wakaenda chumbani na kufanya mapenzi”
Awanywesha watoto sumu kisa maisha magumu
Amesema ilipofika mwezi October mwaka jana Mwanafunzi huyo aligundulika kuwa na ujauzito baada ya kufanyika vipimo shuleni kwa Wanafunzi wote wa kike na alipoulizwa akamtaja Dismas, licha ya kuhukumiwa miaka 30 mshtakiwa ametakiwa pia kulipa fidia ya Tsh. 1,000,000 kwa mwanafunzi huyo baada ya kutoka gerezani.