Mahakama ya wilaya Mkoani Singida imemuhukumu Abduli Bakari (27) kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili.
Hakimu Mfawidhi Robert Oguda ametoa hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 230/2019 ambapo amesema matukio ya vitendo vya ubakaji na mimba katika wilaya ya Singida vimekithiri hali inayochangia mabinti wadogo kupoteza masoma yao bila sababu zozote za msingi.
Aidha amesema ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama mshtakiwa huyo, atakwenda kutumikia miaka 30 jela kwa kosa la kwanza la kubaka na katika shtaka la pili la kumpa mimba amemuhukumu kifungo cha mika 30 jela na makosa yote yanaenda kwa pamoja.
Naye Mwendesha mashtaka wa Serikali amesema kuwa mwezi februari mwaka jana mshtakiwa alimbaka mwanafunzi mwenye umri wa mikaa15 anayesoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari Mudida.
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana, ndipo upande wa mashtaka ulipopeleka mashahidi watano mahakamani ambao walitoa ushahidi uliothibitishia mahakama hiyo bila kutia shaka yoyote kwamba mshtakiwa ndiye aliyembaka mwanafunzi huyo.