Kocha kutoka nchini Ujerumani Ernst Middendorp ametangazwa kuwa mnrithi wa mikoba ya Hans Pluijm ndani ya Singida Fountain Gate yenye maskani yake Singida.

Pluijm anaingia kwenye orodha ya kuwa kocha wa kwanza kukutana na Thank You msimu wa 2023/24 alipopata fursa ya kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Agosti 29 alitangazwa Pluijm kupewa mkono wa asante na Septemba Mosi Middendorp alitangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika na ligi.

Akizungumza baada ya kutambulishwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 64, aliweka wazi kuwa anatambua kuna kazi kubwa ya kufanya na timu hiyo na wanahitaji matokeo.

“Ninatambua ligi ina ushindani mkubwa na kuna wachezaji wazuri kwa ushirikiano nina amini tutapata matokeo na kufikia malengo ambayo tunahitaji”.

Miongoni mwa timu ambazo aliwahi kuzifundisha kwenye bara la Afrika ni pamoja na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Asante Kotoko ya Ghana na St George ya Ethiopia.

Max Allegri: Juventus tumejitafuta, tumejipata
Waliovamia Bunge kisa uchaguzi wakalia kuti kavu