Mwamuzi wa zamani, Mike Dean ametoa maoni yake na kukubaliana na uamuzi uliotolewa juu ya matukio ya mchezo wa ushindi wa Arsenal wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester United, juzi Jumapili (Septemba 03).

The Gunners ilipata ushindi wa dakika za mwisho kupltia kwa Declan Rice na Gabriel Jesus, lakini ingeweza kuongoza mapema kwa penalti baada ya Kai Havertz kuangushwa na Aaron Wan-Bissaka.

Mwamuzi Anthony Taylor aliamua upigwe mkwaju wa Penati, lakini baadae alilazimika kubadili uamuzi baada ya kuangalia picha za marudio ya VAR.

Lakini kwa Dean, uamuzi wa Taylor ulikuwa sahihi hata baada ya kubadilishwa, aliiambia Sky Sports: “Naweza kuona jinsi tulivyofika katika uamuzi sahihi. Mwanzo ilionekana kuwa Penati na kila mmoja uwanjani.

“Lakini kutoka katika upande mwingine, beki hakucheza faulo. Mguu wa Havertz ulimfanya Wan-Bissaka amguse.”

Mwamnyeto, Job wabebeshwa mzigo Stars
Mifumo ufuatiliaji kutathmini miradi programu za Vijana