Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta hakuweza kuficha furaha yake baada ya Arsenal kuishinda Manchester City na kutwaa Ngao ya Jamii juzi Jumapili (Agosti 06).

Washika Bunduki hao walianza kufungwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu England kwa bao la Cole Palmer dakika ya 77.

Lakini Arsenal walifanikiwa kusawazisha mambo kwenye Uwanja wa Wembley dakika ya 101 kwa bao la Leandro Trossard aliyetokea benchi.

Bao la Mbelgiji huyo, ambalo lilisababisha mchezo huo kwenda kwa mikwaju ya Penalti, ambapo Arsenal waliibuka washindi kwa 4-1 na kufanikiwa kutwaa taji la 17 la Ngao ya Jamii.

Kevin De, Bruy Babio Vieira na Rodri wote walikosa Penati.

Kuhusu ushindi huo muhimu Arteta alisema: “Tunajisikia vizuri. Nadhani ni bora zaidi kushinda kombe kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya timu bora zaidi duniani kwa njia ambayo tulifanya.” Arteta pia alimsifia Mlinda Lango Aaron Ramsdale, ambaye aliokoa kwa ustadi Penati ya Rodri.

Mhispania huyo aliongeza: “Yeye (Ramsdale) alikuwa mzuri.

Tunafanya mazoezi ya Penati mara nyingi kwa makusudi kabla ya msimu ili kuwa tayari kwa hili endapo itawezekana. Tulipitia masikitiko dhidi ya Manchester City, kwa mfano, na hatukuzuia lolote kati ya hayo.

“Huo ulikuwa mwelekeo wa kujifunza, ambao wakati mwingine unahitajika ili kupata matokeo sahihi mwishoni. Nadhani alikuwa mzuri sana.”

Fasheni ya mapengo inawalipa jamii ya Warangi
Young Africans yatembeza mkwara Tanga