Baada ya kikosi chake kushindwa kutwaa ubingwa msimu uliopita, Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amefichua kuwa ana lengo la kujenga timu yenye uwezo wa kutwaa taji la Ligi Kuu ya England msimu ujao 2023/24.
Msimu uliopita pamoja na kuongoza ligi hiyo kwa muda mrefu, Arsenal ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City.
Arteta amesema anaamini hivi sasa kujenga timu ya ubingwa anaweza, baada ya msimu uliopita kufanikiwa kurudisha upya makali ya kikosi chake.
“Tayari tumetengeneza upya kikosi. Sasa tupo pamoja na wamiliki (wa klabu) kujenga timu ya ushindi ambayo inaweza kudumu kwa muda mrefu,” amesema.
“Tunahitaji wachezaji muhimu na tutashambulia soko kusajili wale tunaowahitaji,” amesema.
Katika usajili wa majira haya ya kiangazi, miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa kuwaniwa na Arsenal ni kiungo wa West Ham United, Declan Rice.