Millard Ayo ameeleza jinsi ambavyo aliwahi kunaswa kwenye urimbom wa uzuri wa Jakate Mwegelo ambaye aliwahi kushika nafasi ya pili katika shindano la Miss Tanzania 2006.

Mtangazaji huyo wa ‘Aplifaya’ ya Clouds Fm alisema kuwa alianza kudata na Jokate tangu walipokuwa shule wakikutana kwenye daladala ambapo kutokana na kipato, yeye alikuwa anakaa katika nafasi za wanafunzi lakini Jokate alikuwa analipia nauli ya watu wazima.

Jokatee

“Nilikuwa nampenda yaani… ki-girlfriend,” Millard alimwambia Sporah. “Mimi nilikuwa nakaa jikoni na yeye anakaa analipa nauli ya watu wazima. Kalikuwa kapole yaani, na unajua mimi napenda sana mtu mpole. Lakini sijawahi kumwambia,” aliongeza.

Hata hivyo, Millard alieleza kuwa aliendelea kubaki na hisia zake za kutamani Kidoti awe mpenzi wake lakini baada ya miaka kupita walikutana wakiwa wote ni mastaa na kujikuta wanakuwa marafiki wa karibu sana.

Kwa mujibu wa Millard, suala la mapenzi kwake ilibidi liyeyuke ili aweze kuutunza urafiki wa dada na kaka kati yake na mrembo huyo ambaye ana historia kwenye moyo wake.

“Mimi namheshimu sana Jokate kwa sababu wakati tunakutana alikuwa ameshakuwa mdada, anayo maamuzi yake na anaye boyfriend wake. Kwahiyo baadae tukaja kuwa marafiki na unajua tena ukitaka kuutunza urafiki lazima mambo ya mapenzi usiyahusishe,” alisema.

Ukaribu wa Millard na Jokate umewahi kutengeneza tetesi kuwa wawili hao ni wapenzi lakini wao waliukanusha, “ni urafiki wa dada na kaka”.

Hata hivyo, Millard ambaye amesema kuwa anaye mchumba wake ameendelea kumuweka mbali na umma kwa kutomtaja akisema muda muafaka utakapofika atafanya hivyo.

“Kufutwa Sherehe za Siku ya Ukimwi Kumetutia hasara”
Balozi Seif: Dk Shein, Maalim Seif Wamekubaliana Uchaguzi Urudiwe