Kocha Mkuu mpya wa Tanzania Prisons, Fred Felix ‘Minziro’ amesema baada ya kuingia kambini juma hili ameona kuna haja ya kuongeza wachezaji wawili eneo la kiungo na ushambuliaji.

Juma lililopita Prisons ilimsajili Mshambuliaji, Salum Kihimbwa akitokea Dodoma Jiji mwenye uwezo pia wa kucheza kama winga, lakini Minziro amesisitiza anahitaji kupata Mshambuliaji mwingine.

Minziro amesema baada ya siku tatu za mazoezi, sasa anataka kufanya marekebisho eneo la kiungo mkabaji na mshambuliaji.

Pia amesema atawasilisha marekebisho hayo kwa viongozi ili kuhakikisha msimu ujao Prisons inafanya vizuri na kuleta ushindani katika Ligi Kuu.

“Tunashukuru mazoezi yanaendelea vyema na wachezaji wana hali na morali.” amesema Minziro

Minziro amerejea tena Prisons timu aliyowahi kuinoa misimu kadhaa iliopita na kuchukua nafasi ya Abdallah Mohamed ‘Baresi’ aliyejiunga na Mashujaa iliyopanda TPL.

Afya Tip: Njia mbadala za kurudisha hamu ya tendo la ndoa
Mlinda Lango wa Cameroon akamilisha Simba SC