Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), amesema Shilingi Bilioni 3.7 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Majaliwa amesema hayo leo Septemba 18 2020, wakati akizungumza na wakazi wa kata za Mkula na Lamadi wilayani humo akiwa njiani kuelekea Bunda mkoani Mara.
Majaliwa amesema fedha hizo zimetumika kujenga mradi wa maji bomba katika kijiji cha Lukungu ambao ambao tayari umekamilika na kufanya ukarabati wa chanzo cha maji katika mradi wa maji wa Kalemela – Mkulaambao nao tayari umekamilika.
Wakati huohuo, Majaliwa amesema ili kuboresha miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo mpya, shilingi billioni 2.3 zimetolewa kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA), katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Majaliwa pia alitumia nafasi kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli, wagombea ubunge na wagombea udiwani.